• Test
 • Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Bw. John M. Shibuda ( katikati) akizungumza na vyombo vya Habari katika ukumbi wa ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar e salaam Januari 29/2017
 • Mhe. Jaji Francis S. K Mutungi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya kufutwa kwa usajili wa kudumu wa vyama vitatu vya siasa ambavyo ni CHAUSTA, APPT- Maendeleo) na Chama cha Jahazi Asilia leo Novemba 09, 2016.
 • Bi. Theresa Mghanga, Mkurugenzi mpya wa Utawala na Rasilimali watu (wa kati kati kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi mara baada ya ukaribisho katika ukumbi wa mikutano
 • Msajili wa Vyama vya Viasa Mhe. Jaji Francis Mutungi akitoa wito kwa Vyama vya Siasa kutafuta suluhu ya sintofahamu ya kisiasa kwa majadiliano wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari ofisini kwake Agosti 24,2016
 • Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakati wa kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi wa Baraza hilo kilichokutana kujadili hali ya siasa Jijini Dar es Salaam
 • Bw. Sisty Nyahoza , Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa akiwa katika picha ya pamoja na wananchama wa Chama cha ADC mara baada ya kufanya Uhakiki wa chama hicho Julai 18, 2016
 • Aliyekuwa Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa (katikati) Bw. Ibrahim Mkwawa, akikagua nyaraka mbalimbali za Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakati wa uhakiki Juni 27
 • Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bw. Sisty Nyahoza (kulia) akikagua daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha National League for Democratic (NLD) wakati wa zoezi la kuhakiki Juni 27
 • Maadhimisho ya utumishi wa umma, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikisikiliza na kujibu kero za wadau wa vyama vya siasa Juni 24
 • Baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano wa watumishi kusikilizwa changamoto zao Juni 22
 • Mkuu wa Masijala (ORPP), Bi. Galasia simbachawene akipokea taarifa ya marejesho ya gharama za uchaguzi Mkuu 2015 kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa CCM Bw. Stanslaus Mamiro Juni 22, 2016
 • Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Baraza la vyama vya Siasa baada ya kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika April 29,2016 katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
 • Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi wakifuatilia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
 • Waziri wa Nchi ( ofisi ya Waziri Mkuu) Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kil
 • Aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein ameshinda kiti cha Urais kwa asilimia 91.4 kwenye uchaguzi wa Marudio Machi 20, 2016
 • Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi ( Kushoto) akizungumza na mmoja wa wasimamizi wa Uchaguzi wa marudio katika kituo cha kupiga kura cha Nungwi Zanzibar uliofanyika Machi 20,2016
 • Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimemtangaza Dkt Vicent Mashinje kuwa Katibu Mkuu wa mpya wa Chama Machi 12, 2016
 • Viongozi wa ngazi ya kitaifa kutokaTanzania bara na Visiwani katika Sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan Mjini Unguja Januari 12,02013
 • Amina Yakobo, mwakilishi wa Chama cha African Democratic alliance party (TADEA) akiagana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi Jijini Mbeya Novemba 24, 2015 mara baada ya Kikao na Vyama Vya Siasa Kanda ya Nyanda za juu Kusini
 • Picha ya Pamoja ya Msajili wa Vyama Vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi na Viongozi wa Chama cha Demokraisa na Maendeleo ( CHADEMA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini novemba 23,2015
 • Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Bw. Alhaji Mwangi Kundya (katikati) akimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi akifafanua jambo wakati alipotembelea Ofisi za Chama hicho Jijini Mbeya Novemba 23, 2015. Kushoto ni viongozi wa Kanda w
 • Mhe. Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Mbeya Novemba 23, 2015 akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mbeya
 • Bw. Deonatus F.N Mutani mmoja wa waanzilishi wa chama cha Tanzania Patriotic Front (TPF MASHUJAA)( kulia) akipokea cheti cha usajili wa muda kutoka kwa Mhe. Jaji Francis S. K Mutungu, Msajili wa Vyama vya Siasa Novemba 09,2015
 • Mhe. Hamad Rashid, Mgombea Urais kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Zanzibar (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Jaji Francis S. K Mutungi na ujumbe wake walipofika nyumbani kwake katika hatua za kutafuta Suluhu ya mg
 • Bi.Hamida Kibwana Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la UNDP Zanzibar (wa pili kulia)akifafanua jambo Oktobar 30, 2015 kuhusiana na mchango wa shirika hilo kwa Vyama vya Siasa nyakati za uchaguzi
 • Mhe. Jaji Mutungi akizungumza na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Bw.Salum Ali Salum (kushoto) katika ukumbi wa mikutano wa Tume ya uchaguzi Zanzibar Oktoba 30, 2015.Kulia ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Rajabu Baraka Juma
 • Mhe. Maalim Seif na Mhe. Jaji Mutungi wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi kutoka na Ofisi ya Msajili w Vyama Vya Siasa walifika nyumbani kwakeOktoba 30,2015 kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa
 • Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Mhe. Maalim Seif akifanua jambo kwa Msajili wa vyama vya siasa nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi alipofika nyumbani kwake Oktoba 30, 2015 kutafu
 • Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Vuai Ali Vuai (wa pili kulia) akielezea jambo kwa Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi wakati alipofika katika ofisi za chama hicho Oktoba 29, 2015 kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa
 • Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji S.K. Mutungi akipiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wa ngazi za ubunge na udiwani katika kituo cha kupigia kura cha shule ya Msingi Bunge mapema Asubuhi Octoba 25, 2015
 • Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi akiwa katika kikao na Wahariri na Wandishi waandamizi kutoka baadhi ya vyombo vya habari nchini kilicofanyika ukumbi wa ofisi za Bunge jijini Dar es salaam wakijadiliana kuhusu utunzani wa Amani ka
 • Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewateua Bw. Mrisho mpoto (kulia) na Bi. Christina Shusho (kushoto) kuwa Mabalozi wake ambao watabeba ujumbe wa Amani na kuupeleka kwa jamii kuthamini Amani ya Tanzania kwani ni fahari Yetu sote hivyo watanzania waw
 • Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 • Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakati wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika Feb 6, 2014 katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 • Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa Feb 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 • Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad katika picha ya pamoja na wenyeviti wa vyama vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa Feb 6, 2014
 • Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu Dar es salaam.
 • Rais Jakaya Kikwete akitia sahihi kiapo cha msajili mpya wa vyama vya Siasa
 • Msajili mpya wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akitia sahihi baada ya kuapa.
 • Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis Mutungi akiwa na maongezi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mara baada ya kumtembelea ofisi kwake.Kushoto kwake ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Rajabu Baraka Juma
 • Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis Mutungi akiwa na maongezi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mara baada ya kumtembelea ofisi kwake.
 • Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis S.K. Mutungi (kushoto) akiwa na Raisi wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein
 • Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis S.K. Mutungi (kulia) akiwa na Raisi wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein
«
»

Welcome

Karibu kwenye ukurasa wa tovuti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania. Hii ni taasisi ya Serikali inayojitegemea na yenye jukumu la kukuza na kuimarisha mfumo wa siasa ya demokrasia ya Vyama vingi nchini. 
 
 

UJUMBE KUTOKA KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

 

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilianzishwa mnamo mwaka 1992, na Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992.

Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni pamoja na kusajili vyama vya siasa, kugawa ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, kufuatilia mapato na matumizi ya vyama na vya siasa na kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992, Sheria ya Gharama za Uchaguzi Na. 6 ya mwaka 2010 na kuwa sekretarieti ya Baraza la Vyama vya Siasa.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeanzisha tovuti hii, ili kufanya huduma zetu zijulikane kwa umma na kurahisisha mawasiliano kati yetu na wadau. Aidha, tovuti hii inatupa fursa ya kupata maoni na changamoto wanazokumbanazo wadau wetu na wananchi wengine, ili tuweze kuboresha huduma zetu na kujenga uhusiano mzuri na wadau wetu.

Ni mategemeo yangu kuwa, tovuti hii inatakuwa ni chanzo cha kwanza cha habari kuhusu ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Vyama vya Siasa na Demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Vile vile, itakuwa chanzo cha kwanza cha mawasilino na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Ninatoa wito kwa wadau wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na wananchi wengine, kutembelea tovuti hii mara kwa mara, mpate kukujua kazi zilizofanyika, zinazofanyika na zitakazofanyika na utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ujumla

Ahsanteni na karibuni sana

Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

 
 
Follow Us: