JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

JAJI MUTUNGI AWAKUMBUSHA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KUTII SHERIA ZA NCHI
21 Jun, 2018
JAJI MUTUNGI AWAKUMBUSHA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KUTII SHERIA ZA NCHI

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Mutungi amewaasa Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Vyama vya Siasa na Sheria za nchi kwa ujumla.

Wito huo ameutoa kupitia taarifa yake kwa vyombo vya Habari aliyoitoa Juni 20, 2018 akitahadharisha kuwepo kwa tabia ya baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini ambao hutumia vibaya vyombo vya habari, hususani mitandao ya kijamii, kwa kufanya vitendo au kutoa kauli ambazo zinavunja sheria za nchi.

“Ni wajibu wa kila mmoja kuelewa kwamba katika kutekeleza majukumu yao ya kisiasa wanapaswa kuheshimu sheria za nchi wakati wote ili kudumisha na kukuza demokraisa ya vyama vingi na kulinda Amani ya nchi “alisisitiza Jaji Mutungi

Pia Jaji Mutungi ameonya tabia ya baadhi ya Viongozi wa Vyama vy Siasa kutumia vibaya dhana ya Demokrasia na uhuru wa habari kwa kuwataka wale wote wenye tabia hiyo kuiacha mara moja.