Majukumu
Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa yameainishwa katika Sheria ya Vyama vya Siasa nayo ni haya yafuatayo:-
- Kusajili na kufuatilia utendaji wa vyama vya siasa kwa mujibu wa Sheria;
- Kuratibu shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa;
- Kufuatilia mapato na matumizi ya vyama vya siasa;
- Kugawa na kufuatilia matumizi ya fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa vyenye sifa;
- Kutoa elimu ya uraia kuhusu sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa;
- Kuratibu elimu ya uraia inayotolewa kwa vyama vya siasa;
- Kufanya utafiti kuhusu masuala ya siasa na demokrasia ya vyama vingi;
- Kuwa kiungo kati ya Serikali na vyama vya siasa; na
- Kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayohusu vyama vya siasa.
- Pamoja na majukumu yaliyoainishwa hapo juu, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi sura ya 278