Kikao cha Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini za Vyama vya Siasa 29 Mei, 2018
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilikutana na wajumbe wa Bodi za Wadhamini za Vyama vya Siasa katika kikao kilichofanyika leo siku ya Jumanne ya tarehe 29 Mei, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam, kilichokuwa na lengo la kuwajengea uwezo wajumbe hao katika kutekeleza ipasavyo Sheria ya Vyama vya Siasa katika mapato na matumizi ya vyama vyao