JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

mafunzo ya Uangalizi uchaguzi mdogo 22 Septemba 2018
Maafisa wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wanaojiandaa kushiriki katika uangalizi wa kampeni za uchaguzi unaotegemea kufanyika Decemba 2 mwaka huu, wameaswa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Sheria ili kujikita katika kuhudumia Vyama vyote kwa usawa. Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Gharama za Uchaguzi na Misaada Bi. Piencia Kiure wakati akifungua mafunzo ya siku mbili juu ya Sheria za Gharama za Uchaguzi na Maadili ya Vyama vya Siasa kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S. K Mutungi yanayoendelea kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa jijini Dar es Salaam.