Mkutano wa Msajili na viongozi wa kitaifa wa vyama vya Siasa Septemba 19,2018
Jaji Mtungi amesema ni muhimu kujenga vyama kama taasisi imara kwani mtu yeyote kutoka nje anayehitaji kuwekeza katika vyama hawezi kufanya hivyo ikiwa chama kina hati chafu kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 19, 2018 wakati wa mkutano wake na viongozi wa kitaifa wa vyama vya iasa nchini uliofanyika katia ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es salaam.