JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Vitendo vinavyokatazwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi
Ujumbe kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Unakihusu Chama cha Siasa, mgombea nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani na wewe mwananchi..... Msajili wa Vyama vya Siasa anakukumbusha wewe mwananchi ni haki yako kusikiliza sera ili uweze kufanya maamuzi sahihi.... na wewe mgombea na chama cha siasa kipindi hiki cha uchaguzi ni muda wa kueleza sera zako na sio kitu kingine. Kumbuka kipindi cha uchaguzi siyo wakati wa kutoa matusi, kudhalilishana, kugawa watu, kueneza chuki na kuvunja amani Kipindi cha uchaguzi ni wakati kuacha Sera Zako Ziongee!”