Wajumbe Baraza la Vyama vya Siasa Wapongeza Mchakato Uchaguzi wa Viongozi kwa kuendeshwa kwa uhuru na uwazi
Kamati ya kusimamia Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa ikiongozwa na Msimamizi wa Uchaguzi huo, Bw. Sisty Nyahoza wakiwa katuika zoezi la kuhesabu kura wakati wa Mkutano Maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa kwa ajili ya Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Nashera Hotel Mjini Morogoro jana tarehe 23 Julai, 2026. Uchaguzi umekamilika kwa Mhe. Juma Ali Khatibu kutetea kiti cha cha Uenyekiti kwa kupata kura 30 za ndiyo dhidi ya kura moja iliyoharibika huku Makamu wake akiwa ni Mhe. John Mongella ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzzi (CCM) Bara baada ya kupata ushindi wa kura 30 za ndiyo dhidi ya kura moja ya Hapana. ( Picha na ORPP)